Monday, 22 December 2014

Sudan




Rais wa Sudan, Omar Al Bashir amemualika Rais Uhuru Kenyatta kwa ziara rasmi nchini humo kama njia moja wapo ya kukuza uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Waziri wa maswala ya Kigeni nchini Sudan,Ali Ahmed Karti amewasilisha rasmi ombi hilo jijini Nairobi kwa waziri wa maswala ya kigeni nchini, Balozi Amina Mohammed.

Akihutubia waandishi wa habari baada ya kupata mualiko huo, Balozi Amina amesema kuwa ana imani kuwa rais Uhuru Kenyatta atazuru nchini Sudan Hivi karibuni.

Kulingana na Ratba ya Rais Kenyatta ni kuwa huenda akazuru nchini Sudan  mapema mwakani  na baadaye Rais wa Sudan Omar Bashir kuzuru humu nchini.

No comments:

Post a Comment