Monday, 22 December 2014
Al Bashir
Rais wa Sudan Omar al Bashir amekashifu vyombo vya habari vya magharibi hasa vile vya Marekani.
Al Bashir amesema kuwa baadhi ya vyombo hivyo vinatoa picha zisizo sahihi na za uwongo kuhusu hali ilivyo kwa sasa nchini Sudan.
Akizungumzia haya akiwa katika mji wa Khartoum ameongezea kuwa kuharibiwa kwa picha ya nchi hiyo kunaonyesha udhaifu wa vyombo vya habari katika kupasha jamii.
Akimalizia amesema kuwa nchi ya marekani haitimizi ahadi iliyoieka ya kuiondolea nchi yake vikwazo vilivyowekwa tangu mwaka wa 1997 na kuongezwa mwaka mmoja na Rais Barack Obama mwaka mwengine mmoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment