Watu wanne wa kundi la Al Shabab washukiwa kutaka kushambulia basi la abiria eneo la Nyangoro wilaya ya
Witu kaunti ya Lamu.
Walioshuhudia wanasema kuwa watu hao waliabiri basi
hilo kama abiria kisha kushuka bila kujeruhi yeyote, hii ni baada ya kukosa
waliowatarajia kwenye gari hilo.
Comanda wa kaunti ya Lamu Ephantus Kiura alisema
ukosefu wa mtandao ulichangia kwa mawasiliano baina yao na vikosi vya GSU, KDF
na polisi wa kawaida waliopelekwa kwenye mkasa huo kutoa usaidizi.
Hatimaye washukiwa hao walitorokea kwenye msitu ulioka karibu na eneo la mkasa.
No comments:
Post a Comment