Sunday, 21 December 2014

Bungeni



Sheria ya usalama iliyopitishwa bungeni chini ya spika Justin Muturi imezua hoja kali kutoka kwa mrengo wa upinzani wa serekali CORD.

Wakuu wa Cord kama Junet Mohamed na Ababu Namwamba wameeleza kua spika huyo alikuwa muhusika mkuu kutetea mrengo wa Jubilee bungeni humo.

Spika Justin Muturi alijiteteA kwa kusema hajutii maamuzi yake kwani ilimlazimu baada ya chama kimoja kutaka kuharibu mpango wa agenda iliyoratibiwa.  

Justin Muturi aliongezea kwa kusema kuwa unapoamua baina ya pande mbili kutapatikana mshindi na atakaye shindwa na anaona alichukua uamuzi wa busara  kama vile spika mwengine mwenye tajriba angeamua.

No comments:

Post a Comment