Rais wa Sudan, Omar Al Bashir
amemualika Rais Uhuru Kenyatta kwa ziara rasmi nchini humo kama njia moja wapo
ya kukuza uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Waziri wa maswala ya Kigeni nchini
Sudan,Ali Ahmed Karti amewasilisha rasmi ombi hilo jijini Nairobi kwa waziri wa
maswala ya kigeni nchini, Balozi Amina Mohammed.
Akihutubia waandishi wa habari baada
ya kupata mualiko huo, Balozi Amina amesema kuwa ana imani kuwa rais Uhuru
Kenyatta atazuru nchini Sudan Hivi karibuni.
Kulingana na Ratba ya Rais Kenyatta
ni kuwa huenda akazuru nchini Sudan mapema mwakani
na baadaye Rais wa Sudan Omar Bashir kuzuru humu nchini.