Monday, 22 December 2014

Sudan




Rais wa Sudan, Omar Al Bashir amemualika Rais Uhuru Kenyatta kwa ziara rasmi nchini humo kama njia moja wapo ya kukuza uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Waziri wa maswala ya Kigeni nchini Sudan,Ali Ahmed Karti amewasilisha rasmi ombi hilo jijini Nairobi kwa waziri wa maswala ya kigeni nchini, Balozi Amina Mohammed.

Akihutubia waandishi wa habari baada ya kupata mualiko huo, Balozi Amina amesema kuwa ana imani kuwa rais Uhuru Kenyatta atazuru nchini Sudan Hivi karibuni.

Kulingana na Ratba ya Rais Kenyatta ni kuwa huenda akazuru nchini Sudan  mapema mwakani  na baadaye Rais wa Sudan Omar Bashir kuzuru humu nchini.

Zimbwabwe





Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaachisha kazi mawaziri wawili na naibu wa mawaziri watano.
Rais huyo alieko Asia kwa likizo amechukua hatua hii baada ya kutimua wengine saba pamoja na aliyekuwa naibu wake joice Mujuru.
Aidha anasema kuwa tabia na jitihada za kazi yao ni za chini na hazikutarajiwa kuwa hivyo, akiongezea amesema kuwa wanachama hao walikuwa karibu sana na Mujuru ambae anaonekana kuchukua nafasi yake atakapo staafu.
Kwa sasa Rais Mugabe amemteua Emmerson Mnangagwa kama naibu wake

Tunisia




Moncef Marzouki amepinga kutawazwa kwa Beji Caid Essebsi kama rais mpya wa Tunisia kwa kusema kuwa ushindi huwo haukuwa wa kidemocrasia.
Mshindi, Mr Essebsi mwenye umri wa miaka 88 ametoa shukrani kwa Marzouki na wafuasi wake na pia amewaambia wananchi wa Tunisia kuwa ni wakati mzuri kwa wao kushirikiana na kufanya kazi pamoja bila kubagua yeyote ili kuleta utulivu nchini humo.
Itafahamika kuwa uchaguzi huwo ndio wa kwanza wa kidemocrasia tangu kupata kwao uhuru mwaka wa1956.

Al Bashir




Rais wa Sudan Omar al Bashir amekashifu vyombo vya habari vya magharibi hasa vile vya Marekani.
Al Bashir amesema kuwa baadhi ya  vyombo hivyo vinatoa picha zisizo sahihi na za uwongo kuhusu hali ilivyo kwa sasa nchini Sudan.
Akizungumzia haya akiwa katika mji wa Khartoum ameongezea kuwa kuharibiwa kwa picha ya nchi hiyo kunaonyesha udhaifu wa vyombo vya habari katika kupasha jamii.
Akimalizia amesema kuwa nchi ya marekani haitimizi ahadi iliyoieka ya kuiondolea nchi yake vikwazo vilivyowekwa tangu mwaka wa 1997 na kuongezwa mwaka mmoja na Rais Barack Obama mwaka mwengine mmoja

Sunday, 21 December 2014

UCHAGUZI TUNISIA



Moncef Marzouki amepinga kutawazwa kwa Beji Caid Essebsi kama rais mpya wa Tunisia kwa kusema kuwa ushindi huwo haukuwa wa kidemocrasia.

Mshindi, Mr Essebsi mwenye umri wa miaka 88 ametoa shukrani kwa Marzouki na wafuasi wake na pia amewaambia wananchi wa Tunisia kuwa ni wakati mzuri kwa wao kushirikiana na kufanya kazi pamoja bila kubagua yeyote ili kuleta utulivu nchini humo.

Itafahamika kuwa uchaguzi huwo ndio wa kwanza wa kidemocrasia tangu kupata kwao uhuru mwaka wa1956.

ROMA



Klaus Iohannis aapishwa kuwa rais mpya wa nchi ya Roma baada ya kumpiku mwenzake Victor Ponta katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Klaus aliyezoa asilimia 54.5  dhidi ya 45.5 alizopata Ponta alitoa shukrani kwa wananchi wake na kuwaahidi kupigania utowaji na upokeaji rushwa kwa nchi hiyo maskini ya pili chini ya umoja wa bara uropa.

Hata hivyo rais huyo mpya amesema kuwa ushindi wake ulikuwa wa huru na halali