Sunday, 21 December 2014

UCHAGUZI TUNISIA



Moncef Marzouki amepinga kutawazwa kwa Beji Caid Essebsi kama rais mpya wa Tunisia kwa kusema kuwa ushindi huwo haukuwa wa kidemocrasia.

Mshindi, Mr Essebsi mwenye umri wa miaka 88 ametoa shukrani kwa Marzouki na wafuasi wake na pia amewaambia wananchi wa Tunisia kuwa ni wakati mzuri kwa wao kushirikiana na kufanya kazi pamoja bila kubagua yeyote ili kuleta utulivu nchini humo.

Itafahamika kuwa uchaguzi huwo ndio wa kwanza wa kidemocrasia tangu kupata kwao uhuru mwaka wa1956.

ROMA



Klaus Iohannis aapishwa kuwa rais mpya wa nchi ya Roma baada ya kumpiku mwenzake Victor Ponta katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Klaus aliyezoa asilimia 54.5  dhidi ya 45.5 alizopata Ponta alitoa shukrani kwa wananchi wake na kuwaahidi kupigania utowaji na upokeaji rushwa kwa nchi hiyo maskini ya pili chini ya umoja wa bara uropa.

Hata hivyo rais huyo mpya amesema kuwa ushindi wake ulikuwa wa huru na halali


CANCCER



Watafiti  nchini Australia wamegundua kuwa utumiaji wa aina ya dawa za maumivu kama asprini na brufen, zinao uwezo wa kupambana na uchochezi na kupunguza makali ya kansa ya ngozi.

Kulingana na mtafiti mkuu Catherine Olsen dawa hizo za maumivu zinao uwezo wa kuzuia kansa hiyo ya ngozi.

Hii ni baada ya uchambuzi uliofanywa kuzindua dawa hizo ambapo ulipunguza hatari ya aina ya kansa ya ngozi, squamous cell carcinoma kwa asilimia 18  

Lamu




Watu wanne wa kundi la Al Shabab washukiwa kutaka kushambulia  basi la abiria eneo la Nyangoro wilaya ya Witu kaunti ya Lamu.

Walioshuhudia wanasema kuwa watu hao waliabiri basi hilo kama abiria kisha kushuka bila kujeruhi yeyote, hii ni baada ya kukosa waliowatarajia kwenye gari hilo.

Comanda wa kaunti ya Lamu Ephantus Kiura alisema ukosefu wa mtandao ulichangia kwa mawasiliano baina yao na vikosi vya GSU, KDF na polisi wa kawaida waliopelekwa kwenye mkasa huo kutoa usaidizi.

Hatimaye washukiwa hao walitorokea  kwenye msitu ulioka karibu na eneo la mkasa.

Bungeni



Sheria ya usalama iliyopitishwa bungeni chini ya spika Justin Muturi imezua hoja kali kutoka kwa mrengo wa upinzani wa serekali CORD.

Wakuu wa Cord kama Junet Mohamed na Ababu Namwamba wameeleza kua spika huyo alikuwa muhusika mkuu kutetea mrengo wa Jubilee bungeni humo.

Spika Justin Muturi alijiteteA kwa kusema hajutii maamuzi yake kwani ilimlazimu baada ya chama kimoja kutaka kuharibu mpango wa agenda iliyoratibiwa.  

Justin Muturi aliongezea kwa kusema kuwa unapoamua baina ya pande mbili kutapatikana mshindi na atakaye shindwa na anaona alichukua uamuzi wa busara  kama vile spika mwengine mwenye tajriba angeamua.

Tuesday, 21 October 2014

EBOLA

Ebola, ugonjwa jinamizi unaosababishwa na virusi. ugonjwa huu unaua idadi
kubwa ya watu kwa muda mfupi. Kusambazwa kwa ugonjwa huu ni pale mtu
atakaposhika jasho, kinyesi, mate, matapishi, mkojo, damu ama kutumia vifaa
 vya kukata kama wembe wa muathirika.

Ishara zake ni kuumwa na kichwa,koo kukauka,kutapika,kuumwa na misuli,
kuendesha,mwili kukosa nguvu na ishara kubwa ni kuvuja damu kwa mashimo
yote ya mwili

Ilani ni kuwa ugonjwa huu hauambukizwi kupitia hewa.

Thursday, 25 September 2014

DEAD AND THROWN

Likoni, county of Mombasa shocking incident happened when a driller was cleaning a well after a break of some month so that he can come and proceed in drilling it. On the process he came across a dead human body which was killed and thrown in.Red cross members came and removed the body from the well and left it for police to come and carry out their investigation plus taking the body. The body was on clothes which was a trouser meaning he was a he. This shows how security is in need in the area of Likoni.
1