Abiria
waliokuwa wameabiri ndege ya AIR FRANCE iliyosajiliwa kwa nambari 463 iliyokuwa
ikielekea nchini Mauritius kutoka France, wamelazimika kushuka ghafla katika
uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa, baada ya kupatikana kilipuzi ndani ya choo
cha ndege hiyo.
Abiria
473 waliokuwa ndani ya ndege hiyo wamesalimishwa na kufanyiwa ukaguzi alfajiri hiyo
ya saa 2:00, huku wanajeshi wa maji Kenya Navy na maafisa wa kutegua mabomu wakifanikiwa
kuwatia mbaroni washukiwa wawili.
Waziri
wa Usalama Joseph Ngaissery na msemaji wa polisi Charles Owino wametoa kauli
zao kufuatia kitendo hicho cha kigaidi.
No comments:
Post a Comment