Friday, 25 December 2015

KENYATTA NA FAMILIA YAKE WASHEREHEKEA KRISMASI MOMBASA


Rais Uhuru Kanyatta na familia yake akiwemo mke, mama, na watoto wake pamoja na seneta wa Nairobi Mike Mbuvi "Sonko"wamesherehekea siku kuu ya krismasi katika kaunti ya Mombasa.


Rais Uhuru ambaye ziara yake imekuwa ya siri mjini humo, amehudhuria misa ya maombi katika kanisa la Cathedral lililoko katika barabara na Nkruma jijini humo.



SHAMBULIZI LAMU


Wapiganaji wa Al- Shabab wamemuuwa polisi mmoja, baada ya bomu walilotega kulipuka muda mchache baada ya kupita lori la polisi kupita katika eneo hilo lililoko katika barabara ya Bodhei iliyoko katika kaunti ya Lamu.

Inaarifiwa maafisa hao walikuwa wanaelekea katika eneo la Bodhei lililoko katikati mwa kaunti ya Lamu na Garissa kabla ya tukio hilo kutokea.

                                     

KRISMASI


Wakristo kote ulimwenguni wameungana na waumini wengine katika sherehe za kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulingana na maandiko ya dini yao.

Viongozi wa dini hiyo wamehubiri kudumishwa kwa amani, kuzidisha upendo pamoja na kumcha Mwenyezi Mungu ili kuzuia  Mashambulizi yanayotekelezwa na magaidi.


                                 

Wednesday, 23 December 2015

IEBC

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imetangaza tarehe ya uchaguzi mdogo wa Useneta wa kaunti ya Kericho na Ubunge wa Malindi kaunti ya Kilifi kufanyika Machi ya tarehe 7 mwaka 2016.

Wakati huo huo maspika wa mabunge yote mawili Justin Muturi wa bunge la kitaifa na mwenzake Ekwe Ethuro wa Seneti, wametangaza rasmi uwazi wa viti hivyo viliwi.




Viti hivyo vilisalia wazi baada ya aliyekuwa seneta wa kaunti hiyo Charles Keter na mbunge Dan Kazungu kuteuliwa kuwa waziri wa Kawi na Madini mtawalia.

Sunday, 20 December 2015

HOFU ZA BOMU


Abiria waliokuwa wameabiri ndege ya AIR FRANCE iliyosajiliwa kwa nambari 463 iliyokuwa ikielekea nchini Mauritius kutoka France, wamelazimika kushuka ghafla katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa, baada ya kupatikana kilipuzi ndani ya choo cha ndege hiyo.

Abiria 473 waliokuwa ndani ya ndege hiyo wamesalimishwa na kufanyiwa ukaguzi alfajiri hiyo ya saa 2:00, huku wanajeshi wa maji Kenya Navy na maafisa wa kutegua mabomu wakifanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa wawili.

Waziri wa Usalama Joseph Ngaissery na msemaji wa polisi Charles Owino wametoa kauli zao kufuatia kitendo hicho cha kigaidi.

  

Friday, 18 December 2015

RATIBA YA LIGI YA UINGEREZA HII LEO

Ratiba ya mechi zinazotarajiwa kuzaragazwa katika viwanja tofauti katika Ligi ya Uingereza hii leo.

Klabu ya Chelsea huenda ikachuana bila usimamizi wa mkufunzi baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi.


18:00 Chelsea - Sunderland
18:00 Everton - Leicester City
18:00 Manchester United - Norwich City
18:00 Southampton - Tottenham Hotspur
18:00 Stoke City - Crystal Palace
18:00 West Bromwich Albion - AFC Bournemouth
20:30 Newcastle United - Aston Villa

Thursday, 17 December 2015

UBAKAJI

Maiti ya mtoto mwenye umri wa miaka 11 imepatikana ikiwa imekatwakatwa katika nyumba ya mwanaume mmoja anaeshukiwa kuwa mhusika wa kitendo hicho katika eneo la likoni kaunti ya Mombasa.


Mzazi wa marehemu amesema binti yake alitoweka nyumbani kwa muda wa siku tatu bila ya kujulikana alipokuwa, huku wakifanya kila juhudi ya kumtafuta bila mafanikio.

Mshukiwa huyo amejisalimisha katika kituo cha polisi huku wakazi waliojawa na hasira wakimshambulia nusra kumuuwa mbele ya maafisa hao

Saturday, 12 December 2015

SHEREHE ZA JAMUHURI NCHINI

Taifa la Kenya linaadhimisha miaka 52 tangu kujinyakulia uhuru wake kikamilifu kutoka kwa mikono ya wakoloni mnamo mwaka 1963.

Rais wa nne wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mwanawe Hayati Mzee Jommo Kenyatta ataongoza sherehe hizo jijini Nairobi huku magavana wakiongoza katika kaunti wanazoziwakilisha nchini.










Thursday, 10 December 2015

HUMAN RIGHTS DAY

Taifa la kenya limeungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya sherehe za haki za kibinadamu.

Monday, 7 December 2015

JAMAA AGEUKA MBWA

Mwanamke mmoja adaiwa kugeuka mbwa katika kituo cha basi mjini Mombasa baada ya kutoka katika eneo la Mwingi lililoko Ukambani.


Friday, 4 December 2015

WIZI WA PIKIPIKI

Mwanamume mmoja katika eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa ameteketezwa moto baada ya jaribio lake la kumshambulia bodaboda na kumuibia pikipiki yake na pesa alfajiri ya leo kutibuka.