Ndege za moja kwa moja kati ya taifa la Kenya na Marekani
zimeratibiwa kuanza shughli zake kwa miezi miwili endapo bunge litaridhia
mswada wa usafiri wa hewani.
Mamlaka ya usafiri wa hewani KCAA imesema iko katika mikakati ya
kuafikia masharti ya usalama wa hewani, ambayo itapelekea ndege za humu nchini
kuanza safari za moja kwa moja hadi Marekani.
Serikali imetoa muda wa siku 21 kwa wakenya wenye pembe za wanyama pori kuziwasilisha kwa idara husika la sivyo nguvu zitumike dhidi yao.
Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya maafisa wa polisi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kunasa pembe 18 za ndovu zenye thamani ya shilingi milioni 6.4.
Pembe hizo zinazosemekana zililegwa kusafirishwa mjini Bankok nchini Thailand kutoka Mozambique, zilikuwa zimefichwa katika maboxi 22 yaliyodaiwa kubeba madini aina ya Gemstone.
Maafisa kutoka shirika la wanyama pori kws wamemuuwa simba aliyemjeruhi mkazi baada ya kutoroka mbugani kwa kumpiga risasi.
Maafisa hao wamesema wamelazimika kumuuwa simba huyo baada ya jaribio lao la kutaka kumdunga sindano ya kumtoa fahamu kugonga mwamba.
Simba huyo alionekana katika barabara ya Isinya-Kajiado mapema leo akirandaranda kabla ya kumjeruhi mwendesha bodaboda.
Kinara wa mrengo wa Cord Raila Odinga akishirikiana na baadhi ya viongozi wa mrengo wake wa kanda ya Pwani wameitaja barabara moja katika kaunti ya Mombasa jina la mwendazake mwanawe Fidel Odinga.
Ziara ya Raila mkoani Pwani inajiri siku chache baada ya kuhitimika kwa ziara ya Rais Uhuru Kenyatta katika kanda hiyo.