Thursday, 31 March 2016

KIKAO CHA RAIS

Hali ilivyokuwa kabla ya kikao cha rais Uhuru Kenyatta cha kuhutubia taifa katika bunge alasiri ya leo.



WANASHERIA WAAPISHA

Hanan El Kathiri anakula kiapo kwa kutumia Quran katika kuhudumu kama mwanasheria wa mahakama kuu.





MWANA WA BESIGYE NAYE YUPO KINYANG'ANYIRONI

Mtoto wa kiume wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ni miongoni mwa wanafunzi waliojitokeza kuwania urais katika chama cha mijadala katika chuo kikuu cha Oxford nchini Marekani.

KIKAO CHA TAIFA

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa adhuhuri ya leo kuhutubia taifa kuhusiana na hali ilivyo nchini ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Kikao hicho kitakuwa ndani ya bunge la kitaifa, hali ambayo wabunge kutoka upinzani wametishia huenda wakakwepa hotuba hiyo.

Wednesday, 30 March 2016

COURT ACQUITS THUITA MWANGI.



Former Foreign Affairs permanent secretary Thuita Mwangi alongside former ambassador to Libya Anthony Muchiri and former chargĂ© d'affaires in Tokyo Allan Mburu have been acquitted of all charges in relation to the Tokyo embassy scam.

                            

RADIO SALAAM MINUS PRESENTER.

News Presenter and Reporter Douglus Omare famously Mr. Chairman departs Mombasa based Fm Radio Station Radio Salaam for Milele Fm.
                                                  

USAFIRI KUIMARISHA UCHUMI


Ndege za moja kwa moja kati ya taifa la Kenya na Marekani zimeratibiwa kuanza shughli zake kwa miezi miwili endapo bunge litaridhia mswada wa usafiri wa hewani.



Mamlaka ya usafiri wa hewani KCAA imesema iko katika mikakati ya kuafikia masharti ya usalama wa hewani, ambayo itapelekea ndege za humu nchini kuanza safari za moja kwa moja hadi Marekani. 

PEMBE ZANASWA JKIA.

Serikali imetoa muda wa siku 21 kwa wakenya wenye pembe za wanyama pori kuziwasilisha kwa idara husika la sivyo nguvu zitumike dhidi yao.

Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya maafisa wa polisi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kunasa pembe 18 za ndovu zenye thamani ya shilingi milioni 6.4.
Pembe hizo zinazosemekana zililegwa kusafirishwa mjini Bankok nchini Thailand kutoka Mozambique, zilikuwa zimefichwa katika maboxi 22 yaliyodaiwa kubeba madini aina ya Gemstone.

SIMBA WAZIDI KUTOROKA MBUGA JIJINI NAIROBI

Maafisa kutoka shirika la wanyama pori kws wamemuuwa simba aliyemjeruhi mkazi baada ya kutoroka mbugani kwa kumpiga risasi.
Maafisa hao wamesema wamelazimika kumuuwa simba huyo baada ya jaribio lao la kutaka kumdunga sindano ya kumtoa fahamu kugonga mwamba.
Simba huyo alionekana katika barabara ya Isinya-Kajiado mapema leo akirandaranda kabla ya kumjeruhi mwendesha bodaboda.

Thursday, 24 March 2016