Ebola, ugonjwa jinamizi unaosababishwa na virusi. ugonjwa huu unaua idadi
kubwa ya watu kwa muda mfupi. Kusambazwa kwa ugonjwa huu ni pale mtu
atakaposhika jasho, kinyesi, mate, matapishi, mkojo, damu ama kutumia vifaa
vya kukata kama wembe wa muathirika.
Ishara zake ni kuumwa na kichwa,koo kukauka,kutapika,kuumwa na misuli,
kuendesha,mwili kukosa nguvu na ishara kubwa ni kuvuja damu kwa mashimo
yote ya mwili
Ilani ni kuwa ugonjwa huu hauambukizwi kupitia hewa.